SHARE

Read 'Amkeni' Lyrics By Nay Wa Mitego

SHARE

Read And Sing Aloud 'Amkeni' Lyrics By Nay Wa Mitego. The song has been well received by fans in East Africa.

READ ALSO: Read Kudadadeki Lyrics By Nay Wa Mitego

Read 'Amkeni' Lyrics By Nay Wa Mitego Below:

Raisi

Listen to me 

Nitakachokiongea unaweza niona sio mzalendo 

Zalendo zalendo gani 

Nchi inaendeshwa kimagendo 

Wengine mwisho wa wimbo huu mtasema mimi mchochezi 

Kila kitu kipo wazi mama yenu analea wezi 

Ndiyo anafuga wezi hapa kikubwa dua 

Hata report ya CAG hakuna aliyechukuliwa hatua 

Yani kodi kila sehemu na bado mnakopa daily 

Bandari mme muuzia mwarabu na mkataba ndo wamilele 

Najiuliza why Mungu ulimchukua John mapema

Ulimchukua tujifunze au tupate kuhema

Huu mtihani haki ya Mungu mimi nakosa cha kusema  

Kazi yako haina makosa ikikupendeza chukua na hawa 

Media za bongo zimestuck hazina tena ubunifu 

Hazikuzi presenter wapya zinaangalia nani maarufu 

Mh

Na hao maarufu sasa hao machangudoa

Mwenye kisu kikali huyo ndo atakae mng’oa 

Ah

Amkeni nyinyi hakuna elimu ya bure 

Ninachojua mimi elimu ni gharama

Siku zote  nachoamini cha bure akina maana 

Wanatupa elimu mbovu ya bure isiyo na maana 

Na ndo maana siku hizi tunawasomi wajinga sanaa 

Pro ya mama ni kubwa kuliko utendaji wake 

Mabango kila kona 

Wanamdanganya ndege bora kuliko ongezeko la mshahara

Wanamshauri aongeze ndege mashirika yanaendeshwa kihasara 

Ukiwachukua viongozi wetu wakaiongoze marekani 

Na wamarekani waiongoze Tanzania 

Baada ya miaka mitano marekani itafulia 

Kwamba watarudi kuomba msaada Tanzania

Nishatafuta kazi elimu yangu nikakosa 

Nikatafuta kazi ya mshahara mdogo nikakosa 

Hata ya mshahara wa chakula bado nao nikakosa 

Nipo na vyeti nangoga miujiza ya Mwamposa 

Tatizo wasomi wengi na walo fanikiwa hawapendi siasa

Wajinga ndo wanakimbilia 

Tunapata viongozi wajinga uchumi umayumba 

Bongo akili ndogo inaendesha akili kubwa 

Viongozi ni panya road walio vishwa suti 

Na sisi walipa kodi tunawapigia salute 

Nchi imejaa migodi ila tunaongoza kwa dhiki 

Wanatuuliza mbona atuogi na maji walikata wiki 

Nyie wajinga sijawatusi ila nyie ni washenzi 

Na mama ikikupendeza kuhusu mkataba wa bandari 

Usiishie bara peleka na Zanzibari 

Mnauza twiga mzigo wanatupanga mpaka basi 

Wabunge kututetea na ukimya mmepaki basi 

Nguvu kubwa inayo tumika  kumpamba mtandaoni 

Na kwenye media ila huku mtaani hakubaliki na pia hauziki 

Endeleeni na ten zenu zakupeana kila wiki 

Na bunge lenu la mchongo ,spika wa mchongo

Limebaki jina la bunge na vikao vya CCM

Aya tuache masiala turudi kwenye ukweli 

Hivi tunapo elekea tunafaulu hama watu wanafeli 

Miaka miwili tu ilipita tuliishi kwa nguvu ya buku 

Na ilo buku unachagua unga kilo au mchele nusu 

Na sasa mzunguko wa bei ni zaidi ya mara tatu 

Unga kilo buku mbili na mchele ni buku tatu 

Hapa  tu  namkumbuka alisemaga ntamkumbuka 

Okay 

Tuachane na hilo kuna kasumba imezuka 

Sipendi unafki na uchawa 

Simlisema haki sawa 

Ona sasa akikosolewa mnaleta mambo ya jinsia 

Haitoshi kwa wanao kosoa na kesi mnawafungulia 

Nawaona tu mnapotea na wakati mnajua njia 

Aah 

Mnauza twiga bado mzigo anatupanga mpaka basi 

Wabunge kututea na ukimya umebaki basi 

Amkeni nyinyi hakuna elimu ya bure 

Nachojua mie elimu ni gharama 

Siku zote nacho amini cha bure akina maana 

Wanatupa elimu mbovu ya bure isiyo na m,aana 

Ndo maana siku hizi tunawasomi wajinga sana

Related

ADVERTISEMENT