SHARE

Read Zuwena Lyrics By Diamond Platnumz

SHARE

Read And Enjoy Zuwena Lyrics By Diamond Platnumz. The song marks another time Diamond Platnumz has paid homage to Bongo Fleva.

READ ALSO: Diamond Platnumz Signs A New Artist To WCB Wasafi | SEE DETAILS

Read Zuwena Lyrics By Diamond Platnumz Below:

Mhhh!! Habari gani kaka naamini unanisikia

Mimi mzima wa Afya Mama Mungu anasaidia

Toka ulipotuacha Mahututi

Anazidiwa Bibi Presha Presha nae akatangulia

Bado twakuombea ulale salama Pema

Japo Moyoni nina dukuduku

Natamani kusemaaaa

Nisemeeeeee Zile mali husia ulizotuhusia tuligawa Salama

Zuwena Zote Tukampatia tusiwe ndugu lawama Ilaa!!

Zuena Kaka amebadilika Sanaa

Yaan shemlake Bi Zuuh wa leo sio yule wa jana

Natamani Ungemuona Zuwena!!!

Japo ungemuona Zuwena!!!

Kidogo tu ungemuona Zuwena!!!

Ungemuona Zuwena!!!

Ooohh Ungemuona Zuwena!!!

Aahh Zuwena Zuwena!!!

Oohh ungemuona Zuwena Zuwena!!! Mhhh!

Zuwena sasa kawa chotara

Sio tena Cheusi Mangala

Ngozi kaichubua awe Muzungu

Anavuta na Sigara Mara

Boko Mwananyamala

Anachezesha tu miamala Kutwa anaisugua

Kipepe Rungu Tena Peku bila ndala

Aaah Zuwena siku hizi anabandika Kope Zuwena!!!

Zuwena mipasuo kama yote Zuwena!!!

Ooh Zuwena lipa shika tuondoke Zuwena!!!

Aah Zuwena wanamuita cha wote Oooh oooh

Juzi kabebwa na majirani hata hajitambui Zuwena!!!

Yaan kalewa tafarani kautwika Mbwiiiii Zuwena!!!

Zuwena sio tena wa ibada na dini Sadaka chenji asaidie

Siku hizi kageuka pedeshee wa mjini

Kutunza bendi wamsifie

Na lile gari lako urithi wa babu la kulishia Ng’ombe

Siku hizi kama kwato kwenye vilabu linabebea pombe

Mama Dede kitandani hawez hata kutembea

Zuwena ameshindwa hata kuja kumuona panadol kumletea

Natamani Ungemuona Zuwena!!!

Japo ungemuona Zuwena!!!

Kidogo tu ungemuona Zuwena!!!

Ungemuona Zuwena!!!

Ooohh Ungemuona Zuwena!!!

Aahh Zuwena Zuwena!!!

Oohh ungemuona Zuwena Zuwena!!!

Siku hizi kataradadi

Anadanga anakula ndizi kwa maganda

Anajiita JLO

Anadanga anakula ndizi kwa maganda

Eti muzungu mweusi

Anadanga anakula ndizi kwa maganda

Anatunyoosha Baba

Anadanga anakula ndizi kwa maganda

Related

ADVERTISEMENT