SHARE

Turudiane Lyrics by D Voice featuring Lavalava

SHARE

Read and sing aloud Turudiane Lyrics by D Voice featuring Lavalava. The song has been well-received in Tanzania and beyond.

A portrait image of Tanzanian singer, D Voice

Turudiane Lyrics by D Voice featuring Lavalava

Nimekua bubu nimepigwa na butwaa

Mdomo mzito kinywa kama ndondocha

Macho yana magugu sioni mbele najikwaa

Yani ujanja sina nimezorota

Naona joto sijoto baridi sibaridi

Mwili wachoma choma

Naona kichwa kinawaka moto

Moyo unakwenda speed

Yani homa sihoma

Vipimo nmemaliza kwa manguli daktar

Waganga matabibu

Kumbe najilimbikiza maumivu makali

Naongeza maswahbu

Nimezunguka kote Buza na Yombo Dovya

Sijaambulia chochote zaid ya kuchovya chovya

Rudi tuishi sote ujinga tu uliniponza

Jaribu kusahau yote mtima uje kupoza baby fanya..

Turudiane, Turudiane tena

Turudiane.. Tuwe kama zaman

Fanya turudiane, Turudiane tena(Unirudie baby)

Turudiane.. Tuwe kama zamani (Turudiane)

D Voice

Yalopita yamepita sindwele

Rudi tugange yajayo we nmekuzoeaa

Tufanye yamekwisha uje tujenge yambele

Yale tuachane nayo mwenzako najidodea.

Rudi tufunike kombe mwanaharam apite

Tusijali tutaonekanaje kwa ndugu jamaa

Nimekubali kwako kibonde acha tu nidhalilike

Sina habari ata wakisemaje nachotaka furaha

Yale matusi kejeli vijembe

Mafumbo kutupiana yote tufanye yaishe

Najua twapendana kweli sasa ya nini tunazozana..

Rudi penzi tudumishe..

Nimezunguka kote Buza na Yombo Dovya

Sijaambulia chochote zaid ya kuchovya chovya

Rudi tuishi sote ujinga tu uliniponza

Jaribu kusahau yote mtima uje kupoza baby fanya..

Turudiane, Turudiane tena

Turudiane.. Tuwe kama zaman

Fanya turudiane, Turudiane tena(Unirudie baby)

Turudiane.. Tuwe kama zamani (Turudiane)

Read Other Latest Song Lyrics Here

Get Fresh updates as they drop via Twitter and Facebook

Related

ADVERTISEMENT