Read Sio Kwa Ubaya Lyrics By Mwana FA Featuring Harmonize
Read Sio Kwa Ubaya Lyrics By Mwana FA Featuring Harmonize. The song has been well-received by fans in Tanzania and beyond.
READ ALSO: Read Mozzah Lyrics By Aslay
Read Sio Kwa Ubaya Lyrics By Mwana FA Featuring Harmonize:
VERSE 1
Hela sio matamko kwamba kila mtu anazo Zilipo Mwanangu Usilete Mchezo
Kuwaza Hela Hakuna Kwenda Likizo
Hasa wenzangu na mimi ambao hatukuzaliwa nazo
Eti hazileti furaha ukiwa sikiliza shauri yako Sio swala la mjadala hii ndo iwe ramani yako Eeeh pambana ziwe zako
Pigana mwana mpaka wachange jina lako Tunawatolea sadaka, sadaka tunazopata Laana zinatuepuka dua mbaya zinaturuka
Hata ufahamu kwanini wananiita baba roho tisa kama za paka I'm ma brothers keeper
The white collar Don kama Paul Castellano wanatangulia kufunga ila sipotezi mapambano
Usiende mbali kumbuka kuna kurudi mayai yote kapu moja man karibu unabugi
BRIDGE
Moyo wa Champion sioni competition
Mitihani ya maisha hufaulu kwa kwenda tuition
AKA ya ulimwengu nnayekutia fimbo za ugoko ka hukufunzwa na mama ako shauri yako
CHORUS
Mi sina time ya kupoteza ngoma ya mtu siwezi cheza so usiponiona usiulize jua tu niko bize nazichanga si kwa ubaya
Mi sina time ya kupoteza ngoma ya mtu siwezi cheza so usiponiona usiulize jua tu niko bize nazichanga si kwa ubaya
VERSE 2
Ukiwa na siku ya kutafuta na ya kupata ipo ridhiki hatoi baba ako kwamba itakufuata ulipo
Nakutia moyo kukata tamaa mwiko sio lele mama ilibidi mnagombea fito Penda hela usiziabudu usivukwe na
Utu roho yako ya chuma usiache iwe kutu Sheria msumeno lakini haichani dhiki mawe yameiva na mkaa bado umebaki
Pesa hainunui furaha ufukara unanunua nini mi nakimbiza hela mademu mewaachia nyinyi
Hizi si habari za mjini ni habari zangu mimi maisha hayana subtitle sio lazima uniamini Pata hela maadui zako wanune
Usihofu life manigga mipunga ndo nguvu za kiume
Au uendelee kulala ka utakuwa ulichokiota asiye hustle na asile ukija kitaa utatukuta
BRIDGE
Moyo wa Champion sioni competition Mitihani ya maisha hufaulu kwa kwenda tuition
AKA ya ulimwengu nnayekutia fimbo za ugoko ka hukufunzwa na mama ako shauri yako
CHORUS
Mi sina time ya kupoteza ngoma ya mtu siwezi cheza so usiponiona usiulize jua tu niko bize nazichanga si kwa ubaya
VERSE 3
Mi sina time ya kupoteza ngoma ya mtu siwezi cheza so usiponiona usiulize jua tu niko bize nazichanga si kwa ubaya
Kwanza naisha mapema kama naishi Kigamboni dili isiyo na pesa Konde Boy humuoni
Gari imefuka moshi ka nimepaki jikoni na usipumuona Mudi Mnyama ipo kiunoni yeeeh