Read Pita Huku Lyrics By Dulla Makabila
Read Pita Huku Lyrics By Dulla Makabila. The singeli song marks another time that Dulla Makabila has dropped a hit song.
READ ALSO: Dulla Makabila Apologizes To Diamond Platnumz In A New Song Titled "Naacha Muziki" | LISTEN
Read Pita Huku Lyrics By Dulla Makabila Below:
We mama mtu mzima ndoa ingekupa heshima
Ila kutwa mitandaoni ulidate na vitoto
Unadai mmeo ana kitambi hawezi kupeleka moto
Hot stories
Aaah we mama pita huku
Uliaminiwa na kanisa ukaongoza kila misa
Ila ulijiona Mungu mtu kisa una pesa sana
Uliamini ushirikina na kula kondoo wa bwana
Mchungaji pita huku
Kutwa ulitukana hujachokozwa unagombana
Yani unalewa mpaka unajikojolea
Ila suala la sadaka ulikuwa unajitolea
We mlevi pita huku
Najua umekata tamaa ndo maana nakuona umeshika tama
Najua umekata tamaa ndo maana nakuona umeshika tama
Yani kazi yako Udj hilo halipingiki
Ila kila ulipofika muda wa ibada ulizima mziki
We DJ pita huku
We kwanza una laana chumbani kwako kuna mafuta kila kona
Unapenda kwa mpalange
Mtume hataki hata kukuona
Aaah we shoga pita huku
Unapenda kwa mpalange mtume hataki kukuona
Aaah we shoga pita huku
Nikikutazama unatia huruma maana naona hutoboi
Ushawatoa mina na zena na ulivyo fundi hukosei
Nawe dokta pita huku
Yani kufumba kufumbua ukajiona umefika
Sheria ukaipindisha masikini ukawakomesha
Na ukanenepa kwa rushwa
We hakimu pita huku
We mtoto wa kike ila nawe una demu
Na mademu wanakuita shemu
Aaaah inauma sana
Hata baba na mama hawataki hata kukuona
Maisha yako yote laana hauna mashine ila kazi tu kusagana
Tom Boy pita huku
Malaya unafanya mtu anatelekeza mpaka familia
Ada ya watoto wake ikifika kwako unakoga bia
Yani kudanga bongo huridhiki unaenda uturuki
Unakunywa vidonge hata mimba hushiki
Mbele ya shemeji zako unapita na kanga
Malaya ukiamua lako unampa mpaka mganga
We malaya pita huku
Mchawi unafanya watu wanafukuzwa kazi
Wengine unawauwa kwa kuwapa maradhi
Mchawi unawaachanisha mpaka wapenzi
Mchawi unawanyima watu usingizi
Mchawi oooh nakosa cha kuongea usiku unageuka paka mabati unarukia
Mchawi unaua mtu anaacha familia msibani unatokea unalia hadi unazimia
Mchawi ndo chanzo cha umasikini unapita kwenye pembe hivi milango huioni
Na uchawi mkaupeleka usafini Yani Lavalava hata aimbe vipi haonekani
We mchawi pita huku