SHARE

Read Jua Lile Lyrics By Nacha Featuring Stamina Shorwebwenzi

SHARE

Read Jua Lile Lyrics By Nacha Featuring Stamina Shorwebwenzi. The song marks another time Nacha and Stamina have collaborated on a song.

READ ALSO: VIDEO: Nacha - Pombe

Read Jua Lile Lyrics By Nacha Featuring Stamina Shorwebwenzi Below:

Oya za siku nyingi mambo vipi 

Huonekani mzee wangu au majukumu 

Ya kinchi 

Bwana weee si unajua maisha yetu 

Tunasaka kwa tabu 

Tukaenjoy wavuvi camp 

Bado unapanda daladala 

Nunua ndinga ata mkweche

We ishu sio ndio ewura wamepandisha wese 

Kwa hiyo ukipandisha kodi na uchumi nao unapanda 

Hiyo GG msee wangu Bet Over na Under 

Hivi ile mirabaha wasanii wanapata kweli na 

Kama wanapata inawafaidisha au kejeli 

Mmmh kaka mbo ni mengi

Nyie acheni kuna mtu kapiga hit 

Afu kapewa buku ten

Mi nna swali kuhusu soka au nikiuliza 

Kwa mada ntakuwa natoka 

Hivi mchezaji wa muda wote kwa

 hapo Bongo 

Ni nani au ni Kibu 

Ahahaha acha utani 

Oya maisha yanachanganya 

Sometimes yanatia wazimu 

Unakuwa mkulima na ulisoma 

Sayansi kim 

Mbona kawaida mzee bado unashangaa haya 

Watu wamesoma journalism afu kazi 

Anapewa chawa 

Kuna vitu vinachanganya naomba unijibu kimoja

Hivi tanesco na dawasa ni ndugu wa baba mmoja 

Aaaah sio ndugu ila kimtindo wanafanana maana 

Wote wanakata utasema wanashinda 

Jua lile jua lile jua lile litelemke mama

Jua lile jua lile jua lile litelemke mama 

Jua lile jua lile jua lile litelemke mama

Jua lile jua lile jua lile litelemke mama 

Mwanaume ana mwanaume je unafahamu 

Au usimuliwe 

Dah bwana ametwaa jina lake lihimidiwe 

Unahisi ukasaidia alafu ukapost picha 

Hapo sina majibu kasome mathayo sita 

Oya we dereva eeeh hii gari si ina mziki 

Piga amapiano tukichafue kwenye seat 

Ndo tatizo lenu wabongo ndo maana mziki wenu haukui 

Kutwa kuwacopy wa naija 

Wengi wenu hamjitambui 

Sawa sahivi tuna tuzo pongezi kwa TMA 

Tunapiga hatua na muziki unapanda bei 

Au ulizionaje tuzo una lolote la kuongea 

Nilishangaa tuzo ya heshima kupewa alozigomea 

Wasanii wabongo wana chuki wanaminyana 

Ndo maana hata endorsement nyingi ni za kujuana 

Bongo nyoso mzee dili nyingi haziko live

Unaweza kuta sidiria isitangazwe na Masha Love 

Oya huko Uturuki kuna nini 

Nasikia limekuwa chaka la wengi 

La dada wengi wa mjini 

Dada zako si unajua wanapenda sana pay 

Unaweza kuta Uturuki wanafata Othman Bey 

Jua lile jua lile jua lile litelemke mama

Jua lile jua lile jua lile litelemke mama 

Jua lile jua lile jua lile litelemke mama

Jua lile jua lile jua lile litelemke mama 

Local players wanalipwa kima cha chini sa kwanini 

Au wengi uwezo wao ni duni

Wengi wanakesha kitambaa 

Afu unataka walipwe sawa 

Siku zote foreigner ana thamani juu ya mzawa 

Wizi wa mitandak umepungua ipongezwe TRA 

Sio mchezo bado TRA kushusha bei 

Hivi ulihesabiwa Sensa 

Ndio nilihesabiwa 

Ila wabongo dili hadi vishkwambi viliibiwa 

Matokeo ya Form Four madogo wengi wametusua 

Hivi hii ni ishara ya elimu yetu kukua 

Yes of course 

Elimu yetu siku hizi inakua 

Ila nna swali mbona wanaofaulu 

Wengi wa kishua 

Na vipi kuhusu hali ya nchi 

We unaiyona uko sawa 

Mmmh mmh acha uchama 

Au unataka kutugawa 

Mana kwa wapinzani naona mwamba karudi 

Mama anaupiga mwingi wewe magoli ya vichwa 

Ka Giroud 

Jua lile jua lile jua lile litelemke mama

Jua lile jua lile jua lile litelemke mama 

Jua lile jua lile jua lile litelemke mama

Jua lile jua lile jua lile litelemke mama 

Jua Lile - Nacha Ft Stamina Shorwebwwenzi

Related

ADVERTISEMENT