SHARE

Read Dunga Mawe Lyrics By Kontawa

SHARE

Read Dunga Mawe Lyrics By Kontawa. This is Kontawa's second release in 2023 and it is making waves in Tanzania.

READ ALSO: Read Sikuachi Lyrics By Kontawa Ft Maua Sama

Read Dunga Mawe Lyrics By Kontawa Below:

Anaitwa Dunga Mawe 

Mwanangu wa Utoto 

Katika kitu nakumbuka 

Alipitia changamoto 

Mwanangu Dunga mawe alikuwaga kiboko 

Na sura yake kutishia watoto 

Oya huyo mwanangu alikuwa msela 

Ashawahi kufungwa akatoroka jela 

Maisha yake visanga yaani mpela mpela 

Asa ngoja niwape movie ilo lilikuwa trailer 

Kuna kipindi Dunga Mawe si alipata mwali 

Tukaenda hadi ukweni sikutoa mahari 

Baada ya vitu kukamilika tulivyopewa mwali 

Akamvizia baba mkwe akamuibia mahari 

Alianza kuvuta bangi na miaka saba

Ulivyofika wa nane akaanza kukaba 

Sababu ya hali ngumu kakosa msaada 

Hakuwahi kuwa na mama wala huyo baba 

Ndugu wa karibu wa kumpa faraja 

Mali alizoachiwa na wazazi wake kadhulumiwa   

Aaah aaaah 

Aaaaah dunga mawe

Aaaaah Aaaaah 

Anaitwa dunga mawe 

Aaaaah Aaaah 

Mwanangu dunga mawe 

Ukimletea unyonge lazima aruke nawe 

Bora ukabwe na tonge ila sio dunga mawe 

Utafanya kitu gani ili umfanye apagawe 

Kashaoga matusi mpaka akaamua anawe 

Siku dungamawe akiamka vizuri 

Tena ukamkuta mwenye mood 

Anaweza agiza bia mbili af akakupa mia mbili akasema kwamba change inarudi 

Demu wake dunga mawe alikuwa na mimba

Yapata kama miezi tisa 

Kwa kuwa pesa ya uzazi ilimshinda 

Ikabidi awe anapiganisha 

Akamwambia mpenzi wake kuwa amepata safari 

Anaenda kupambana ili mambo yawe shwari 

Na atakaporudi watakwenda hospitali 

Kumbe alipanga kwenda kuiba huko sehemu za mbali

Ndipo akakamatwa na watu wenye hasira kali 

Wakamshushia kipigo 

Kipigo juu ya kipigo 

Na mwisho wakamchoma na mipira ya magari 

Anaitwa dunga mawe 

Aaaaah Aaaah 

Mwanangu dunga mawe

Anaitwa dunga mawe 

Aaaaah Aaaah 

Mwanangu dunga mawe

Alianza kuvuta bangi na miaka saba

Ulivyofika wa nane akaanza kukaba 

Sababu ya hali ngumu kakosa msaada 

Hakuwahi kuwa na mama wala huyo baba 

Ndugu wa karibu wa kumpa faraja 

Mali alizoachiwa na wazazi wake kadhulumiwa   

Aaaaah Aaaah 

Anaitwa dunga mawe 

Mwanangu dunga mawe

Anaitwa dunga mawe 

Aaaaah Aaaah 

Mwanangu dunga mawe

Dunga Mawe - Kontawa

Related

ADVERTISEMENT