Coke Studio Africa Imezindua List Ya Wasanii Kwa Msimu wa 2019
Kampuni ya Coca-Cola imeyaweka wazi majina zaidi ya 25 ya wasanii wenye vipaji toka barani Afrika ambao watashiriki kwenye msimu mpya ujao wa ‘Coke Studio Africa 2019’.
Wasanii na watayarishaji wa muziki kutoka Kenya, Tanzania, Uganda, Ethiopia, Zambia, Zimbabwe, Msumbiji, Nigeria na nchi zingine kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika ambao watakuburudisha kwa mwaka ujao, kuanzia mwezi Februari 2019, ambapo kipindi kitakapo anza kuruka kwenye kioo cha televisheni yako kote barani Afrika. Kwa mara nyingine tena, wapenzi wa kipindi watapata kushuhudia msisimko wa mchanganyiko wa muziki, marudio ya nyimbo za zamani, na utengenezwaji wa nyimbo mpya.
https://www.youtube.com/watch?v=96Cbv2trKbQ
Kutoka Tanzania msanii nyota wa bongo flava na mshindi wa tuzo ya BET Rayvanny pamoja na mwanadada mwenye sauti nyororo ‘Nandy’ wataungana na kubariki kipindi kwa mara ya pili. Baadhi ya washiriki wapya wenye msisimuko kwenye kipindi ni Harmonize ambaye alitamba na kibao chake “Kwangaru” na Juma Jux, mkali wa muziki wa R&B na msanii kutoka Mdee Music, Mimi Mars.
Hot stories
Kutoka Kenya, Moji Short Baba atapata nafasi ya kushiriki Coke Studio Africa kwa mara ya kwanza akiwa na Naiboi, kwa sasa anatamba na kibao chake cha “2 In 1” na Nguli wa muziki wa kufoka foka (Hip-Hop) Khaligraph Jones, ambaye hivi karibuni ametwaa tuzo ya kuwa mwana muziki bora wa Hip-hop barani Afrika mwaka 2018 katika tuzo za AFRIMMA, atarudi kwa mara ya pili katika msimu huu mpya.
Uganda watawakilishwa na baadhi ya wasanii kama mshindi wa tuzo nyingi mwanadada Sheebah, akirudi kwenye msimu kwa mara ya pili. Mahlet, Bisrat, Abush Zekele, Yared Negu na Rophnan Nuri watatoka Ethiopia.
Ladha ya burudani toka Magharibi mwa Afrika italetwa na watayarishaji wakali wa muziki, GospelOnDeBeatz na nyota wa muziki nchini Nigeria Skales na Rudeboy (alikuwa akiunda kundi la P Square) watakavyo ling`arisha jukwaa kwa utumbuizaji wa hali ya juu na vibao matata.
Utayarishaji wa Coke Studio Africa 2019 unaendelea, kwa nyimbo za kushirikiana za wasanii na waandaaji wa muziki watakao tengeneza muziki utakao waunganisha watu kutoka barani Afrika. Itahusisha zaidi ya nyimbo halisi 10 zilizotengenezwa na mtiririko wa kipekee kwa msimu chrisimass kwa mwezi huu wa Dec 2018 kutoka coke studio Afrika. Msimu huu unao subiriwa kwa hamu utakuwa ukiadhimisha aina mbali mbali za muziki na tamaduni. Itakuja pamoja na kuwa chanzo cha kusheherekea maudhui ya kiafrika na muziki, kutanabaisha hadithi na muunganiko ambao hupaswi kuukosa.