Paka Na Panya (Derby) Lyrics by Roma Mkatoliki featuring Latifah
Roma Mkatoliki Lyrics
Read, sing aloud and enjoy Paka Na Panya (Derby) Lyrics by Roma Mkatoliki featuring Latifah. The song is currently making waves in East Africa
READ ALSO: Read Nipeni Maua Yangu Lyrics By Roma Mkatoliki Ft Abiudi
Read Paka Na Panya (Derby) Lyrics by Roma Mkatoliki featuring Latifah below:
Naona Gap kubwa kati ya paka na panya
Hii si ni derby sasa mbona siasa za kugawanya
Sisi je nyie ni Tom mnajiona Hilfiger eeeh
Kisa mna power na money mnajiona mambwiga
Mtaani kuna njaa paka acha na sisi
Nyanya imekuajiri leo sokoni haishikiki
Tunaishi ili tule tunakula ili tuishi
Si alileta elimu bure mbona wasomi haizalishi
Mzee mbabe untouchable mkali ka Mugabe
Hakuiva na Manji wenye ganji akasema akabwe
Panya wakafyata mkia wakapotea wenye ngebe
Acha kumpinga ukimsema unanyea debe
Hakua mlevi wa uhuru kunyata kama kalewa
Labda kama madaraka yanalevya alolevyewa
Sometimes hivi vyeo vina hangover
Lake gang wakasukuma wakatakeover
Ni yeye alileta swaga za ku-fly over
Ila ni yeye democracy alii-bend over
Sahani vyombo vya panga na vyombo vya dola alitumia anavyotaka kutuchapa na hii bakora
Na si kila mfuga makucha hawezi ogopa kurarua
Kwa Lissu aliona matunda na mwili sio chandarua
Walojidai wazalendo waliisoma namba kirumi
Ukikosoa miundombinu tu umehujumu uchumi
Wakazaliwa chawa wafata upepo ka bendera
Walojifanya sugu walienda jela
Watu wakakiita chuma na hakikuwa na huruma
Na hakikuwa na njia za panya mipango yote ilibuma
Bado vita havina suluhu na kupona ni Majaliwa
Sikuweza kuisema pombe ningejua ningepaliwa
Siku Paka akishika mwambie Panya tunataka Katiba
Hatuogopi hizi shida tutapita hata kama kuna miba
Siku Paka akishika mwambie Panya tunataka Katiba
Hatuogopi hizi shida tutapita hata kama kuna miba
Huyo nyau nyau nani atamfunga paka kengele
Huyo nyau nyau nani atamfunga paka kengele
Kuwatesa panya ndio sifa za paka shume
Huyo nyau nyau nani atamfunga paka kengele
Huyo nyau nyau nani atamfunga paka kengele
Eyoo paka alitawala huu msitu wa serikali
Panya ndo sisi kapuku hatuna hali
Wasiwasi maisha yetu ya mitego katiba ndo ilimpa nguvu huyu paka mwenye ego
AKA donstone paka the DOD
Vipi ashikwe na kiu na maziwa ndo kodi
Kwa panya hakuna minofu na ziliadimika tii
Alitubana tuwe na njaa kwa utii tuseme please
Mtaani kuna njaa hakunali si ye kidume
Tabia ya kuwatesa panya ndo sifa za paka shume
Kwenye runinga alivimba paka alijiona simba
Paka alifanya alichotaka hata angestaafu si ana kinga
Unamgusa vipi na ana jeshi lilimlinda alipoambiwa sio la hapa kula kiugali nikashiba
Na sio Sinza hadi Mafinga hofu ilijaa giza nene
Wanaharakati walimsaka Beni toka saa nane
Kwenye damu ya Akwilina walilipa damu hatujui aliyempiga risasi naamini yuko kazini
Zaidi nani sasa nyie au wadai Katiba nchini
Au kwa vile panya angekuwa paka angefanywa nini
Okay kwani aliyemteka Roma si ndo alivamia mawingu
Je nani alimteka Mo nioneshe aliyepigwa pingu
Bado vita havina suluhu na kupona ni Majaliwa
Sikuweza kuisema pombe ningejua ningepaliwa
Siku Paka akishika mwambie Panya tunataka Katiba
Hatuogopi hizi shida tutapita hata kama kuna miba
Siku Paka akishika mwambie Panya tunataka Katiba
Hatuogopi hizi shida tutapita hata kama kuna miba
Huyo nyau nyau nani atamfunga paka kengele
Huyo nyau nyau nani atamfunga paka kengele
Kuwatesa panya ndio sifa za paka shume
Huyo nyau nyau nani atamfunga paka kengele
Huyo nyau nyau nani atamfunga paka kengele
Hakuishi mbali feri so samaki so shida
Mbele ya panya mwenye njaa akala mnofu bila mwiba
Na alitembea na pesa si jeuri ukiwa na kipato
Yaani tungesema suu New York ingehamia Chato
Aliweza kulinda madini na ukuta sawa UKAWA nao wakataka UKUTA wao wa power
Aaah kwa vile panya sa ukuta wa nini hawa
Paka alimwaga cheche panya tukapagawa
Tukaanza skia skendo mara kidoti ndo bebe
Si ana mkwanja akaanza kununua mandege
Mtoto wa kambo akapewa toy ya Dar alichezee
Si akaanza kupora mali hajui fainali uzee Eeeh
Dogo alikuwa na chuki hakuogopa Mungu wala Mbingu
Genge lake la bunduki si akayavamia mawingu
Nani alimiliki genge la paka wasiojulikana
Akatwadhibu hadi sisi Panya Road ttulioshindikana
Panya hadeki kayatimba hana birthday wala keki
Unapokwepa mtego huu mbele sumu kudadeki
Paka katuziba mdomo kwa mikwara tuwe mabubu
Panya buku mbichi CAG akakatwa sharubu
Tukashinda ndani ya mashimo bado hewa kaidhibiti
Na ukitoka nje kusema eeh eeh unaitwa msaliti
Mi nikaanza kugonga nyagi kuondoa maweru maweru
Na ukipinga hoja zao eti umetumwa na beberu
Na ukipinga hoja zao eti umetumwa na beberu
Ila sio kila panya alipata hiki kichefu chefu
Wale panya wa Lumumba siku zote wako safe
Mpira wao refa wao na tume ndo timu yao
Na mabao ya maradona ndo maana kombe ni lao
Ila kuna panya wa Kigoma haeleweki hatabiriki
Kuna wenzie wanagoma ila yeye anawasaliti