SHARE

Read Machozi Lyrics By Stamina Shorwebwenzi

SHARE

Read Machozi Lyrics By Stamina Shorwebwenzi. The song is Stamina's first release in 2023 and it is expected to make waves.

READ ALSO: Stamina ft. Maua Sama - Nalewa Leo

Read Machozi Lyrics By Stamina Shorwebwenzi Below:

Oy niaje mwamba samahani nakusumbua 

Naomba usikate simu taratibu utanijua 

Nampigia mke wangu naona hapokei simu 

Ila najua umelala nae sorry na kukata stimu 

Na unanijua na unajua si ni wazazi 

Naumia kuona Wanangu wanalala na dada wa kazi 

Na usiulize namba yako nimeitoa wapi 

Naomba uskize mi ni mumewe wa ndoa na chati 

Kwanza nikupe pongezi we mjasiri

mi kulala na mke wa mtu siwezi 

Unapata nguvu ipi kuipa hayo mamlaka hayo

mume wake yu hai hajafa haja pa talaka 

Alafu naskia na sound umechoka sana ndio

mshamaliza round ya kwanza au sio mwana 

Wakati mi nalala mito we unaenjoy unamkunja kama kiko 

Vipi mtamu eeh kanona eeh 

Nagharamika bro sijui kama unanisoma aisee 

Najua unampenda sababu unamhudumia ukitaka

nikuachie bro uone jinsi nnavyoumia 

Kama kidume cha mbegu kesho nikuletee watoto uwalee 

Na Mke wangu unipunguzie msoto inaniuma 

Nimemhudumia nimempa thamani zamani

nakuhakikishia ungemwona haungemtamani 

Kama anasema ndoa imekuwa daah changamoto 

Au anasema tumeachana anabaki tunalea watoto 

Sorry salio inakata anaweka vocha nakupigia ili unipe

simu niongee naye huyo mshenzi wa tabia 

Kama binadamu nina moyo sio chumba naumia 

Machozi yanitoka nashindwa vumilia 

Natamani niondoke hata kwenye hii dunia 

Maana heshima yangu we umeshindwa nitunzia 

Unaniumiza moyo eeeh 

Akili yangu haisomi eeeh 

Umenishusha thamani eeeh 

Nadharauliwa mtaani eeeh 

Pole sana kwa uchovu pole kwa kazi nzito

ya kubeba pombe ya ndovu 

Najua ulipanga unidanganye boya lako kuwa party

illisha late ukalala kwa shosti ako 

Kukuita malaya sitoweza umenizalia watoto

ila heshima unaipoteza 

Japo mambo unayofanya kiasherati we sio smart 

Umesahau una familia au na watoto huwataki 

Okay tuseme sikuridhishi kitandani anayetoa

kodi ya meza hapa nyumbani ni nani? 

Unadhani watoto watakuwa tu sex yetu 

Au nikikosa hela utalishwa na bwana Yesu 

Zile make up kusuka wanna saluni 

Ungezipata wapi nisingekaza kisa uni 

Hata kama sio handsome nilitimiza majukumu 

Sasa huyu atakuwa nini zaidi ya Kukulisha ndumu 

Wazazi waliposema kuwa tukapime DNA 

Nilisema wamezeeka hawa wazazi TZA 

Sahivi naelewa kila nikiwacheki watoto sura yangu

inakuja inaondoka changamoto 

Ukirudi nyumbani chukua kilicho chako 

Tena ikibidi nenda na watoto wako 

Nauonea huruma huo mfuko wako wa uzazi 

Ungekuwa mfuko wa kawaida ningeshaubebea viazi 

Kama binadamu nina moyo sio chumba naumia 

Machozi yanitoka nashindwa vumilia 

Natamani niondoke hata kwenye hii dunia 

Maana heshima yangu we umeshindwa nitunzia 

Unaniumiza moyo eeeh 

Akili yangu haisomi eeeh 

Umenishusha thamani eeeh 

Nadharauliwa mtaani eeeh 

Machozi - Stamina Shorwebwenzi

Related

ADVERTISEMENT