Read Nawaza Lyrics by Barnaba
Read and sing aloud Nawaza lyrics by Barnaba. The song has been well received by fans in Tanzania and East Africa in general.
READ ALSO: Read Rockabye Lyrics By Barnaba Classic
Read Nawaza Lyrics by Barnaba below:
Yele yele yele Waveja wowo
Waveja wowo Waveja wowo
Tajiri rafiki yake pesa
Masikini rafiki yake uhai
Najiuliza yupi mwenye maana
Yule niliompenda jana
Ama wa leo Ama atakaekuja
Kuna muda najiuliza maswali
Wapi niliko sahihi wakati niliopo
Ama niliopita ama niendako
Nichagulieni majibu
Mwingine analilia kuolewa
Mwingine analiliaga talaka
Yupi yupo sahihi
Mwingine anachoma ubani
Yule anadate na jirani
Wakati ana mume ndani
Nakumbuka mama alinisihi
Mwanangu kua uyaone sio magorofa
Unaweza panda ngazi na kushuka
Maisha tambala bovu
Walio wengi wachovu
So chunga sana
Sukari imepanda bei buku mbili
Mchana umepitaga sini dili
Haya yaya
Maisha gheto mabovu
Walio wengi wachovu
Ye wowo
Tunaungaunga mtaani
Life la mtaani gumu
Usitamani vingi vinapita
We ni mwanadamu kidogo chako ridhika
Hujui mwenzako wapi katoka eeeh
Dear God show me the good way
Dear God read me the right way
Nataka fanya vingi
In my life nataka niwe mwema
In their eyes
Binadamu walimkana Yesu
Wewe ni nani
Punguza kujifanya mwenye imani
Wakinuna nawe nuna pia
Wakicheka nawe cheka pia
Mind your business hatulazimishani
Huwezi kuwa mwema kwa kila mtu
Unanikosea alafu unataka nifanye utu
Roho mbaya haijengi
Ila inaepushaga mengi
Maisha ya Bongo yani popote kambi
Mtoto mdogo anambeba
Mwenye kitambi
Kwa heshima alitakiwa
Amwite baba huyo
Kwa phonebook amemsave baby huyo
Maajabu ya Musa haya
Neno urafiki na unafiki
Vimetofautiana herufi moja tu
Just be careful
Kuwa makini na unaosema unawaamini
Usijejutiaga mwenzangu na mimi
Somebody told me
Tafuta pesa Monday
Sio siku ya kazi
Na tukizipata tusifundishane
Kula bata
Hujanisaidia kutafuta so
Punguza ushauri sasa
Sukari imepanda bei buku mbili
Mchana umepitaga sini dili
Haya yaya
Maisha gheto mabovu
Walio wengi wachovu
Ye wowo
Tunaungaunga mtaani
Dear God show me the good way
Dear God read me the right way
Nataka fanya vingi
In my life nataka niwe mwema
In their eyes